Hii ni hali ya dawa kushindwa kuua/kutibu vimelea vya magonjwa iliyokusudiwa kuua pindi dawa hiyo inapotumiwa kutibu ugonjwa husika.
USUGU WA DAWA UNASABABISHWA NA NINI?
Kushindwa kwa dawa kutibu ugonjwa/ kuua vimelea vya magonjwa utokana na matumizi ya dawa yasiyo sahihi ambayo upelekea vijimelea vya magonjwa kujiwekea kinga ya kuuliwa na dawa.
YAFUATAYO NI MATUMIZI YA DAWA YASIYO SAHIHI
- Kutomaliza dozi ya dawa uliyopewa kutibu ugonjwa husika (Hii inajumuhisha pia kuacha kutumia dawa mara tu unapohisi nafuu)
- Kutumia dawa bila ya kufanya vipimo ili kujua unasumbuliwa na ugonjwa gani ili utumie dawa sahihi
- Kutokufuata maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa kama ulivyoelekezwa na mtaalamu wa afya
- Kuchangiana dawa na mtu mwingine(Hii upelekea kupunguza dozi kwa mtu aliyekuwa anatumia ile dawa pia na wewe utakuwa hujatumia dozi kamili
- Kutumia dawa isiyosahihi kutibu ugonjwa husika, (Mfano Kutumia dawa ya kutibu ugonjwa unaosababishwa na Bakteria wakati unaumwa ugonjwa unaosababishwa na Virusi)
MADHARA YA USUGU WA DAWA
- Kuongeza gharama za matibabu
- Kukaa hospitalini kwa muda mrefu
- Uweza kusababisha kifo kutokana na kushindikana kwa Ugonjwa kutibika
NINI UFANYE KUZUIA USUGU WA DAWA?
- Hakikisha unamaliza dozi ya dawa uliyopewa
- Husitumie dawa bila kufanya vipimo kujua unasumbuliwa na ugonjwa gani ili upate dawa/tiba sahihi
- Tumia dawa kama ulivyoelekezwa na mtaalamu wa afya
- Dawa uliyopewa itumie pekee yako, Husichangiane dawa na mwenzako
NB: DAWA INATIBU IWAPO ITATUMIKA KWA USAHIHI NA IPASAVYO
Comments
Post a Comment